Posts

Showing posts from May, 2014

kukombolewa ktk nafsi

Nilikuwa ninafanya huduma sehemu fulani ndipo akanijia ndugu mmoja na kuniambia kuwa anahitaji msaada wangu. Nikaaanza kujitetea, maana hapo mahali nilikuwa nikitumika chini ya mtumishi mwingine, aliyekuwa anaiongoza hiyo huduma. Mpendwa huyu alinisihi sana kiasi nikaguswa ikabidi nimsikilize. Mpendwa huyu alikuwa ni mama mmoja aliyeteseka sana katika maisha yake bila kujua tatizo ni nini na akiishia kwenda kwenye maombi kwa miaka mingi sehemu mbalimbali bila mafanikio. Ndipo aliponijia na kunieleza, “mtumishi naomba uniombee.” Nikamwuliza nikuombee nini? Kwa kuwa yeye alikuwa muwazi, akanambia mtumishi mimi naona Mungu hajibu maombi yangu.   Nilimhoji mama huyu mambo fulani fulani lakini niligundua katika mahojiano naye anabidii ya kwenda kanisani, maombezini lakini hajawahi kukua kiroho yaani hana badiliko katika maisha yake; anakwenda kanisani kwa mazoea tu maana amekuta wanaomzunguka wanakwenda kanisani lakini hajui kwa nini hasa anakwenda kanisani.   Kw...

maombi

  MAOMBI   Bibilia ndio kitabu pekee kinachotuelezea vizuri juu ya sala/maombi. Ni lazima Yesu atajwe katika maombi yoyote na pia kwa sababu ndio jina kuu lipitalo majina yote.   FALME   MAMLAKA   WAKUU WA GIZA   MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO Sala nzuri ni ile inayotoka kwa msukumo mkubwa unaotoka katika moyo   yaani nafsi. Moyo unatakiwa uwe safi na usiwe na majeraha yoyote ndio utapata msukumo wa kuomba.   MAOMBI NI NINI?   Maombi ni mawasiliano kati ya mwanadamu na Mungu. Kila mwamini anaweza kuomba. Kitu pekee kinachohitajika katika maombi ni nidhamu. Tunahitaji ushirika wa kila siku na Mungu kwa njia ya maombi. Efeso 6:12. Tunapotaka   kuwasiliana na Mungu vitu vinatushambulia kwa sababu maombi sio mawasiliano tu bali maombi ni vita. Wakati mwingine tunapotaka kuomba falme, mamlaka na wakuu wa giza na majeshi ya pepo wa baya hutuzuia kwa sababu hiyo huwafanya ...
  MAOMBI   Bibilia ndio kitabu pekee kinachotuelezea vizuri juu ya sala/maombi. Ni lazima Yesu atajwe katika maombi yoyote na pia kwa sababu ndio jina kuu lipitalo majina yote.   FALME   MAMLAKA   WAKUU WA GIZA   MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO Sala nzuri ni ile inayotoka kwa msukumo mkubwa unaotoka katika moyo   yaani nafsi. Moyo unatakiwa uwe safi na usiwe na majeraha yoyote ndio utapata msukumo wa kuomba.   MAOMBI NI NINI?   Maombi ni mawasiliano kati ya mwanadamu na Mungu. Kila mwamini anaweza kuomba. Kitu pekee kinachohitajika katika maombi ni nidhamu. Tunahitaji ushirika wa kila siku na Mungu kwa njia ya maombi. Efeso 6:12. Tunapotaka   kuwasiliana na Mungu vitu vinatushambulia kwa sababu maombi sio mawasiliano tu bali maombi ni vita. Wakati mwingine tunapotaka kuomba falme, mamlaka na wakuu wa giza na majeshi ya pepo wa baya hutuzuia kwa sababu hiyo huwafany...