kukombolewa ktk nafsi
Nilikuwa ninafanya huduma sehemu fulani ndipo akanijia ndugu
mmoja na kuniambia kuwa anahitaji msaada wangu. Nikaaanza kujitetea, maana hapo
mahali nilikuwa nikitumika chini ya mtumishi mwingine, aliyekuwa anaiongoza
hiyo huduma. Mpendwa huyu alinisihi sana kiasi nikaguswa ikabidi nimsikilize.
Mpendwa huyu alikuwa ni mama mmoja aliyeteseka sana katika
maisha yake bila kujua tatizo ni nini na akiishia kwenda kwenye maombi kwa
miaka mingi sehemu mbalimbali bila mafanikio. Ndipo aliponijia na kunieleza,
“mtumishi naomba uniombee.” Nikamwuliza nikuombee nini? Kwa kuwa yeye alikuwa
muwazi, akanambia mtumishi mimi naona Mungu hajibu maombi yangu.
Nilimhoji
mama huyu mambo fulani fulani lakini niligundua katika mahojiano naye anabidii
ya kwenda kanisani, maombezini lakini hajawahi kukua kiroho yaani hana badiliko
katika maisha yake; anakwenda kanisani kwa mazoea tu maana amekuta
wanaomzunguka wanakwenda kanisani lakini hajui kwa nini hasa anakwenda
kanisani.
Kwa
jinsi yoyote ile ni vema kujiuliza, wewe msomaji mwanadamu unapokeaje neno la
Mungu ambacho ndicho chakula cha Roho? Chakula ambacho kinarejesha afya ya roho
na mwili, mafanikio ya kiroho na yakimwili, maendeleo ya kitumishi na kimaisha,
badiliko yanayopelekea kukua kiroho, kuvunja nira kule ulikokamatwa na kuona
kama ndiko sahihi, kukata kamba za uovu, kuachiwa huru kwa walioonewa,
kuangusha ngome na kadhalika?
Mama
huyu baada ya kumchunguza niligundua alikuwa ni “Nafsi mfu.” Niliamua
kumfundisha mama huyu somo la NAFSI. Somo hili la Nafsi mfundishaji akifundisha
kiusahihi anayefundishwa hupokea Baraka za ajabu na hata kuuona uthamani wake
tena! Nafsi inaweza kuibwa,kutekwa,kufungiwa,kuzikwa,kutumikishwa na kadhalika.
Mambo yaliyotokea:
Kufunguliwa
kwa Nafsi. Nafsi ilipofungwa, ufahamu
ambao muda mrefu ulifungwa ulifunguliwa. Mama alikua kiroho. Kumbuka ndugu
msomaji kuwa nafsi ikifungwa hata maisha ya mtu kwa sehemu kubwa huwekwa njia
panda, sababu nguvu za mtu katika utendaji zimeshikwa kule kwenye nafsi yake.
Mfano
hai ni huyu mama ambaye kwa miaka kumi na nane alikuwa hajawahi kupata kazi,
ambapo alikuwa akitunzwa na mumewe… sasa amepata kazi, ikiwa ni pamoja na
kujiajiri mwenyewe! Alikuwa na kiwanja ambacho hakijawahi kuleta badiliko
lolote hapo awali, lakini sasa mpaka kitabu kinaenda mitamboni kaweka msingi wa
nyumba ikiwa ni pamoja na kuingiza bomba la maji.
Kifungo
hiki cha nafsi hakikumkamata yeye peke yake, ni mpaka katika familia. Watoto
walikuwa na taabu ya ada shuleni ambapo lilikuwa kama janga la kifamilia,
lakini baada ya kufunguliwa upande ule wa nafsi tatizo likaisha mpaka katika
kusomesha; watoto wanasoma vizuri sasa tofauti na zamani. Mama huyu kwa sasa
amekuwa ni mtumishi wa Mungu ambaye analiishi neno la Mungu na Mungu akizidi
kumkirimia mambo mema makuu ambayo hakupata kuyajua zamani hizo amen.
KUKOMBOLEWA KATIKA NAFSI
NAFSI NI NINI?
Nafsi ndiye mtu kamili aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu. Ni wewe
halisi, kwa lugha nyepesi ni mtu wa ndani asiyeonekana ambaye ndiye mwenye
maamuzi yote juu ya maisha ya mwanadamu. Nafsi ina uwezo mkubwa kama kufunga
ufahamu ama kuufungua. Kwa hakika nafsi yako na yangu zimebadili vitu vingi.
Nafsi imebadilisha maisha ya mwanadamu. Jinsi ulivyo sasa na
misimamo na maamuzi yako vilivyopelekea ufanikiwe ama ushindwe vinatokana na
nafsi ilivyofanya maamuzi huko nyuma na ikibidi inavyofanya maamuzi sasa. Hebu
tuone machache kuhusu mifano ya nafsi kule inakofanyia kazi zake
zinazodhihirishwa machoni ijapo nafsi yenyewe haionekani katika macho:-
i.
Katika Maisha
ii.
Katika Kazi
iii.
Katika Biashara
iv.
Katika Familia
v.
Katika
Maisha ya ndoa
Matokeo ama niseme mwelekeo wa vitu vyote nilivyoviorodhesha
hapo juu, bila shaka vinahusu nafsi. Hebu tuone mtu ili awe mtu lazima awe na
mambo haya matatu au vitu hivi
vitatu kama kielelezo kinavyoelezea hapa
chini:
Aina Mbili za NAFSI
1. Nafsi mfu
2. Nafsi hai
Ziko aina mbili za nafsi, katika hizo lazima mojawapo iwe kwa
mtu. Haiwezi kutokea mtu mmoja akawa na zote mbili. Kwa nini haiwezekani? Kwa
sababu ya ule mfano usemao nuru na giza haviwezi kukaa pamoja, kila penye nuru
giza halitakuwepo na palipo na kiza ni wazi nuru haipo. Aina hizi mbili za
nafsi zinajibu hoja na mfano huu kuwa kila palipo na dhambi maana yake ni kuwa
hakuna utakatifu na vivyo hivyo palipo na utakatifu uovu haukai.
Lakini katika hoja ya utakatifu na dhambi, dhambi inaruhusu
mchanganyo, lakini utakatifu unataka kujitegemea wakati wote. Haya tuzione aina
hizi mbili:-
1.
Nafsi Mfu: Nafsi mfu ni nafsi ya mtu aliyefungwa (ufahamu). Mtu
mwenye nafsi hii anaweza akawa na bidii ya kuhudhuria ibadani kila wakati
lakini hajawahi kukua kiroho, hana badiliko katika maisha yake na hawezi kuwa
na mabadiliko kamwe. Anakwenda kanisani kwa mazoea lakini hana neno la Mungu
hata chembe moyoni mwake. Huyu ni mfu, mtu wa ndani ameshakufa; mtu huyu wa
ndani ndiye anayeitwa nafsi hai.
NAFSI MFU HII
(HAJUI CHOCHOTE YUPO KATIKA UTUMWA)
2. Nafsi Hai: Nafsi ni mtu aliyebadilishwa maisha
na Yesu. Tunamwita kiumbe kipya, yaani kazaliwa upya. Mpendwa msomaji, uhai wa
nafsi ni suala la kiimani kwamba mtu kapata neema ya kuhubiriwa Neno kwa njia
yoyote ile iwe ni kwa ushuhuda-kashuhudiwa, au kahubiriwa, ama kafundishwa!
Uhai ni ile hali ya kutambuliwa na Mungu kuwa mtu yu salama katika maisha ya
sasa na yale yajayo, tunaita maisha ya milele!
3.
Comments
Post a Comment