maombi
MAOMBI
Bibilia ndio kitabu pekee kinachotuelezea vizuri juu ya sala/maombi. Ni
lazima Yesu atajwe katika maombi yoyote na pia kwa sababu ndio jina kuu
lipitalo majina yote.
FALME
MAMLAKA
WAKUU WA GIZA
MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA
ROHO
Sala nzuri ni ile inayotoka kwa msukumo mkubwa unaotoka katika moyo yaani nafsi. Moyo unatakiwa uwe safi na usiwe
na majeraha yoyote ndio utapata msukumo wa kuomba.
MAOMBI NI NINI?
Maombi ni mawasiliano kati ya mwanadamu na Mungu. Kila mwamini anaweza
kuomba. Kitu pekee kinachohitajika katika maombi ni nidhamu.
Tunahitaji ushirika wa kila siku na Mungu kwa njia ya maombi. Efeso
6:12. Tunapotaka kuwasiliana na Mungu
vitu vinatushambulia kwa sababu maombi sio mawasiliano tu bali maombi ni vita.
Wakati mwingine tunapotaka kuomba falme, mamlaka na wakuu wa giza na
majeshi ya pepo wa baya hutuzuia kwa sababu hiyo huwafanya wakristo wengi
kushindwa kuomba.
Maombi si kitu rahisi na ndio maana watu wengi hushindwa kuomba kwa
sababu maombi ni namna ya kushindana na
adui, kabla ya kuomba ni lazima ujitakase kwa kuomba toba.
Maombi ni mawasiliano lakini pia ni vita, kwa hiyo inatupasa sisi
kusoma neno la Mungu litutoa mahali
tulipo na tuhimarike na kutujenga kuweza kupigana vita na adui.
Lakini hata kama maombi ni vita, ni njia yetu sisi kumiliki. Si kila
wakati ni wa maombi ya kufunga bali kuna wakati mwingine wa kula na kushiba na
kumtukuza Mungu.
Kwa kuwa maombi ni vita inatupasa kubadili mbinu kila wakati, hivyo
kama wanamaombi tunatakiwa kubadili mbinu za uombaji au kupambana kila mara.
Mara nyingi unapokuwa kwenye mazungumzo ya kawaida mwili hauchoki, lakini
unapotaka kuingia kuomba mwili huchoka na usingizi hujaa machoni kwa sababu ya
vifungo vilivyo jaa nafsini mwako ambavyo
vinasababisha kufanya maamuzi ambayo nia na hisiaa vimezuia. Yoh 3:16,
Rumi 5:8, 8:32, 1Yoh 4:9.
Ili uweze kuomba na majibu yaweze kuonekana au kupatikana ni lazima ni
lazima uwe na nguvu ya Mungu, na pia kama waombaji tunatakiwa tufike eneo
ambalo tutajitambua.
KUNA NJIA MBILI ZA MAWASILIANO NA MUNGU
Kila muamini anaweza kuomba lakini lazima awe na nidhamu. Ushirika kila siku na Mungu kwa njia ya
maombi ni kufunga na kuona hali ya kweli yaani kuona badiliko la kweli.
Hatutakiwi kufanya kosa.
Tuishi maisha ya kufanya toba. Ni kitu kinachohitaji kuadabishwa, ni
kitu kinachohitajika kutimiza matumaini.
Kuadabishwa ni kupewa adhabu kwa waliyofanya waliopita kwa kutumia
nguvu, maana yake kushurutishwa. Huna nguvu ya mwilini ya rohoni utashindwa.
Waefeso 6:12, Mathayo 12:29.
Tunaposema tunawasiliana na Mungu falme na mamlaka na nguvu za giza
zinaibuka na kutufanya tusiweze kuwasiliana na Mungu. Kila mwanadamu anataka
kuwasiliana na Mungu, maombi ni vita na adui ukitaka kufanya maombi ni lazima
uakikishe kwamba nafsi yako imejaa neno la Mungu na sio la kupapasa.
Unaweza ukaudhuria kipindi vizuri kula neno la Mungu, vita vinaanza
pale unapopiga goti uanze kuomba ama kuwasiliana na Mungu. Mara kishindo
kimelia mlangoni mara mlango unagongwa, mara miayo mingi. Maombi sio kitu
rahisi, ni namna ya kushindana na kitu tusicho kiona. Watu wengi walifikiri
maombi ni kula ugali mezani. Maombi kama ni maombi mazuri ni lazima uombe toba
utakaswe (maombi ya toba).
Kumbe maombi ni vita ni lazima tupigane na falme na mamlaka. Wakati
unapoomba usipige magoti karibu na kitanda maana vinaleta uvivu. Ukishaona
unaomba unasogelea kochi au kitanda jua hapo hamna maombi, kama maombi ni vita
basi jua sisi wanadamu ni wapiganaji. Mathayo 12:29 ni lazima umfunge mwenye
nguvu, yaani maana yake katika hilo ni lazima umfunge mkuu wa anga ambaye
anazuia maombi yasifike kwa baba.
Kwa sababu hiyo kama ujamfunga huyo mwenye nguvu utashindwa kuwasiliana
na Mungu. Maombi ya vita si ya mtu dhaifu bali maombi ya vita ni ya mtu mwenye
nguvu. Ndio maana majambazi yanapoenda kuiba wanakuja wengi maana wanakuwa na
silaha za kutosha, wapo wabomoaji wa haraka na wapo waingiaji wa haraka kuingia kuiba. Kwenye
ulimwengu wa roho wanaweza kukuingizia kaneno kadogo kakaleta mchafuko.
Na inaonyesha ni jinsi gani ulikuwa hujapambana vizuri katika maombi.
Ungekuwa umekaa vizuri katika maombi yasingekuwapo maneno maneno. Au unakuta
mtu anataka kufanya maombi lakini ndani ya nafsi yake kumejaa mikataba,
maagano, mazindiko ya kimizimu, majini, pepo, uganga, uchawi wa kila aina.
Maombi ni njia ya kumiliki na kutawala. Kama mtu hawezi kuomba maana yake
hawezi kumiliki. Hatuwezi kufanya maombi
kama hizi roho zinatawala ndani mwako au ndani yetu kama mizimu, uchawi n.k.
Comments
Post a Comment