kukombolewa ktk nafsi
Nilikuwa ninafanya huduma sehemu fulani ndipo akanijia ndugu mmoja na kuniambia kuwa anahitaji msaada wangu. Nikaaanza kujitetea, maana hapo mahali nilikuwa nikitumika chini ya mtumishi mwingine, aliyekuwa anaiongoza hiyo huduma. Mpendwa huyu alinisihi sana kiasi nikaguswa ikabidi nimsikilize. Mpendwa huyu alikuwa ni mama mmoja aliyeteseka sana katika maisha yake bila kujua tatizo ni nini na akiishia kwenda kwenye maombi kwa miaka mingi sehemu mbalimbali bila mafanikio. Ndipo aliponijia na kunieleza, “mtumishi naomba uniombee.” Nikamwuliza nikuombee nini? Kwa kuwa yeye alikuwa muwazi, akanambia mtumishi mimi naona Mungu hajibu maombi yangu. Nilimhoji mama huyu mambo fulani fulani lakini niligundua katika mahojiano naye anabidii ya kwenda kanisani, maombezini lakini hajawahi kukua kiroho yaani hana badiliko katika maisha yake; anakwenda kanisani kwa mazoea tu maana amekuta wanaomzunguka wanakwenda kanisani lakini hajui kwa nini hasa anakwenda kanisani. Kw...
God bless you.
ReplyDeletethank you.God may bless you man of God
ReplyDelete