JINSI MKRISTO ANAVYOPATIKANA 

Ukristo siyo jina au dini au dhehebu lolote - Kuna mambo mengi yanayotufanya tuwe kama kristo alivyo kusudia tuwe nayo ni haya yafuatayo-: Ukimkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi wako unapaswa kuwa mkristo wa kweli, ukristo haurithiwi wala haufuatishi ukoo. ZIKO HATUA 3 ZA KUMPATA MKRISTO 1. HATUA YA KWANZA NI KUAMINI NA KUKIRI - Ukiri una maneno mawili i. Ukiri kama unamwamini Kristo kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako ii. Ukiri kama toba – unatubu juu ya uovu wako wote Rumi 10:17 - Ili uamini ni lazima usikie neno sahihi la Kristo kusikia ndiyo mwanzo wa kumkiri Kristo. - Imani chanzo chake ni kusikia neno la Mungu, kile unachokisia chenye kuleta wokovu ni kile kinachotoka kwenye kinywa cha Kristo Yesu mwenyewe. Mfano:Yesu aliwaambia wanafunzi wake jiangaliaeni jinsi msikiavyo Rumi 10:9-10 Kukiri kwa kinywa kutoka ndani ya moyo hakuna wokovu kama hujaamini kutoka ndani ya moyo wote. Moyo wako ukihukumiwa utamkiri Yesu kwa Kinywa. Imani unayokiri lazima iwe imeambatanishwa na moyo ndipo unaweza kukiri uhalisi wa moyo na si vinginevyo. 2 korint 4:1-6 1 Kor 1:21 Swala la kuokoka ni kujitoa sadaka Mungu hataki sadaka nyonge mtu hawezi kuokoka kwa kukirishwa maneno . Hajiwezi mtu huyo anauwezo wa kukubali chochote. 1 Thesa 5:9-10 Tunaokolewa tukiyashika sana maneno ya Mungu Taufanye imara wito wa wokovu kwa neno lake. Lk 8:12 Mtoto anapozaliwa anahitaji kukua katika kulishwa chakula kizuri na husika. 2. UTAKASO KATIKA NENO : Neno la Mungu ndilo pekee Lenye uwezo wa Mkumtakasa mtu. Ili awe Mkristo wa kweli, Yohana 15:3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. Neno la Mungu likija linakuja na Nguvu ya Utakaso Delivarence ya Ukweli ni ktk Neno la Mungu - Neno husafisha uovu wote Efeso 5:25-26 25. Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; 26. ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; 27. apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa. Neno linafanyika maji linatakasa, Yohana 17:17 Ezekiel 36:26-2725. Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. 26. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. 27. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda. Ebrania 4:12. Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. 13. Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu. 14. Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. Kol 3:16. Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Neno linaachilia roho wake juu yetu huwezi kumpokea Roho Mtakatifu bila neno lake

Comments

Popular posts from this blog

kukombolewa ktk nafsi

maombi